Lionel Messi wa FC Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid tumekuwa tukiwafahamu kwa uwezo wao wa kuvunja rekodi kadhaa katika soka na nyingine wakiziweka wao ambazo kwa kawaida wengi wetu tumekuwa tukihisi ni ngumu kuvunjwa katika soka. November 23 naomba nikusogezee rekodi 5 kutoka katika mtandao wa www.sportskeeda.com ambazo hadi kufikia June 2015 Ronaldo na Messi walikuwa wanapewa nafasi ya kuzivunja katika msimu wa 2015/2016.
1- Ronaldo na Messi wanatajwa kuwa na nafasi ya kuvunja rekodi ya ufungaji wa magoli mengi katika fainali za klabu Bingwa Ulaya kwa msimu wa mwaka 2015/2016 kama watajituma zaidi, kwa sasa rekodi ya ufungaji wa magoli mengi katika mchezo wa fainali ya michuano ya Ulaya inashikiliwa na wachezaji nguli wa zamani wa Real Madrid Ferenc Puskas na Alfredo Di Stefano wakiwa na jumla ya magoli 7 kila mmoja. Ronaldo amewahi kufunga magoli katika fainali mbili za Ulaya mwaka 2008 na 2014 huku Lionel Messi akiwa amefunga pia katika fainali mbili mwaka 2009 na 2011.
2- Ronaldo na Messi wanatajwa na mtandao wa www.sportskeeda.com kuwa na nafasi ya kuvunja rekodi ya kufunga magoli mengi katika hatua ya makundi ya michuano ya klabu Bingwa Ulaya. Kwa sasa rekodi hiyo ya ufungaji wa magoli mengi katika hatua ya makundi inashikiliwa na Raul mwenye jumla ya magoli 53, Ronaldo hadi sasa ana magoli 41 wakati Messi 44 hivyo Ronaldo anaweza vunja rekodi hiyo kama atafunga magoli 13 na Messi 10 katika hatu ya makundi msimu wa 2015/2016.
3- Wote Ronaldo na Messi wanaweza weka rekodi ya kufunga goli la mapema zaidi katika mechi za klabu Bingwa Ulaya, rekodi ambayo inashikiliwa na Roy Makaay aliweka rekodi hiyo mwaka 2007 akiwa na FC Bayern Munich alifunga goli sekunde ya 10.12 katika mechi dhidi ya Real Madrid.
4- Mastaa hawa wote ni wakali wa ufungaji wa hat-trick ila wanatajwa kuwa na nafasi ya kuweka rekodi ya ufungaji wa hat-trick ya mapema zaidi, rekodi ambayo inashikiliwa na Bafetimbi Gomis aliiweka akiwa na Olympique Lyonnais ya Ufaransa alifunga dakika ya nane ya mchezo dhidi ya Dinamo Zagreb mwaka 2011, wakati Ronaldo hat-trick yake ya mapema alifunga mwaka 2013 dakika ya 27 dhidi ya Galatasaray na Messi dakika ya 22 dhidi ya Arsenal mwaka 2010.
5- Viwango vyao vya ufungaji vipo juu na wote wanaweza kufunga magoli mfululizo, Messi na Ronaldo wote walikuwa wanatajwa kuwa na uwezo wa kuweka rekodi ya ufungaji magoli katika mechi za michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mfululizo, rekodi ya ufungaji magoli mfululizo hadi sasa ipo chini ya muholanzi Ruud van Nistelrooy aliyemudu kufunga goli 9 katika mechi 9 mfululizo wakati yupo Man United msimu wa mwaka 2002/2003.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.