Kesi imeendelea Mahakama Kuu Mwanza leo November 24 2015, bado ni mwendelezo wa ishu ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Geita, Alphonce Mawazo… CHADEMA ilipata agizo kutoka kwa Mkuu wa Polisi Mwanza kuhusu kuzuiwa kuaga mwili wa kiongozi wao huyo aliyeuawa.
Ishu ikaenda Mahakamani jana na leo nina mengine kutoka Mahakama Kuu Mwanza >>> “Leo asubuhi tumepata ruhusa ya Jaji wa Mahakama kufungua kesi ya kudai haki ya kuzikwa marehemu Mawazo Mwanza.. tumefungua kesi mchana ambapo tumepeleka maombi matatu, kwanza tupate amri ya Mahakama inayotengua zuio la Mkuu wa Polisi Mwanza la kuzuia shughuli za uagaji wa mwili wa Mawazo isifanyike hapa Mwanza.”- John Mallya, Wakili wa CHADEMA.
Maneno mengine ya John Mallya haya hapa nje ya Mahakama >>> “Ombi la pili ni kuiomba Mahakama itamke kwamba zuio hilo ni batili na kinyume cha sheria… Ombi la tatu ni kuomba Mahakama ikataze Mkuu wa Polisi Mwanza kujishughulisha na jambo lolote kuhusu mazishi na kuaga mwili wa Mawazo.”
“Kesi imefunguliwa kwa hati ya dharura sana na itaendelea kesho saa tatu kwenye eneo la wazi, wananchi watapata fursa ya kusikiliza kesi hiyo.”- John Mallya.
Sauti ya John Mallya hii hapa, kutoka nje ya Mahakama Kuu Mwanza leo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE