Asubuhi yako inaendaje mtu wangu? Inawezekana uchambuzi wa magazeti @CloudsFM umekupita, kama hukuzipata zote zilizosikika kwenye kuperuzi na kudadis nilizozirekodi zote ziko hapa unaweza kuzipitia kufidia zilizokupita.
Usitishwaji wa Sherehe za Uhuru kwa mwaka huu na Rais Dk. John Magufuli za pongezwa, huku utendaji wake unaendelea kuwafurahisha watu wengi, watendaji wa Serikali waanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli la kufanya usafi siku ya Uhuru December 9 huku wasomi wakitaka Rais asilegeze kamba.
Agizo la kufuta safari za nje za Mabalozi na Rais Dk. John Magufuli lazua vikwazo vikubwa kwenye utekelezaji wake huku baadhi ya vikwazo hivyo vikiwa Idadi ndogo ya Balozi, Ukomo wa madaraka ya Mabalozi na Mabalozi kutokuwa na utaalamu.
Mahakama Kuu kanda ya Mwanza jana ilitupa pingamizi la Serikali la kuitaka itupilie mbali kesi ya kutaka kuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA, Geita, Alphonce Mawazo na kutoa fursa kwa familia yake kufungua kesi ya msingi.
Ziepita siku kumi toka Rais Dk. John Magufuli aanze makazi yake Ikulu katika kijiji cha Chamwino, Dodoma ila kasi yake ya utendaji kazi imeelezwa kuleta sura mpya ya maisha katika kijiji hicho na toka ujio wa Rais Magufuli mambo mengi kijijini hapo yamebadilika.
Viongozi wa Kiroho nchini wameiomba Serikali ya awamo ya tano kuhamisha ofisi za Wizara zote na kuzipeleka mjini Dodoma ili kutoa fursa ya maendeleo kwenye mikoa mingine ya jirani, kutokana na jiji la Dar es salaam kujaa na uwingi wa watu.
Kiongozi wa Kanisa la Kikatoliki duniani, Papa Francis anatarajiwa kuwasili Kenya leo jioni kwa ajili ya ziara ya siku tatu nchini humo.
Kusikiliza uchambuzi wa stori zote za magazeti kwenye #PowerBreakfast bonyeza play kwenye hii sauti hapa chini.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE