Siku moja baada ya Rais wa Tanzania kuweka headlines kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwa raia wa Kenya, Rais Uhuru Kenyatta ameingia kwenye headlines za aina hiyo baada ya kufanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri la Kenya kwa kuchukuwa maamuzi ya kuwapiga chini Mawaziri wote ambao Wizara zao zinakumbwa na kashfa nzito za ufisadi!
Kama ilikuwa haijakufikia mpaka muda huu basi ikufikie kuwa uamuzi wa Rais Uhuru Kenyatta umekuja siku moja baada ya kutangaza kuwa tatizo la ufisadi Kenya ni tishio kubwa kwa kitaifa hilo na kuahidi kufanya mabadiliko hivi karibuni kama Rais anayeshikilia ofisi.
Vitu vimetendeka, na baadhi ya maamuzi yaliyofanywa na Rais Uhuru Kenyatta siku ya jana ni pamoja na kuongeza idadi ya Wiazara kutoka Wizara 19 hadi Wizara 20 kwa kile alichodai kuwa ni kuzisaidia Wizara kutekeleza majukumu yao kwa ubora zaidi pamoja na kufanya uchaguzi mdogo ndani ya Wizara hizo.
Mawaziri waliokumbwa na kashfa za ufisadi walijiondoa kwenye Wizara zao na sasa wanakabiliwa na kesi za kujibu Mahakamani huku wengine kama Waziri wa Ugatuzi, Anne Waiguru alijiondoa madarakani kutokana na kashfa zilizoweka headlines kubwa Kenya, za kununua kalamu ya moja ya BIC kwa zaidi ya Tzs. 200,000/- za Kitanzania!
Maamuzi haya ya Rais Uhuru Kenyatta yameibua mjadala mkubwa kwa Wakenya na kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, baadhi wakionekana kufuraishwa na kitendo hicho, huku wengine wakihoji maamuzi ya Rais wao.
Nimefanikiwa kuzinasa baadhi ya hizi tweets za Wakenya kwenye Twitter na kuziweka hapa chini…
>>> “Nina matumaini na #CabinetReshuffle mpya, kikwazo kikubwa ni #Wario kwenye michezo. Harambee Stars ilikuwa mchezo wa kuigiza sasa Riadha utakuwa mchezo wa kuigiza“. <<< @LotanSalapei.
Kama ilikupita, hapa chini ipo full video ya Hotuba ya Rais Uhuru Kenyatta kuhusiana na maamuzi yake ya kulivunja Baraza la Mawaziri la Kenya.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE