Usiku wa Jumatano ya November 25 kulichezwa michezo nane ya muendelezo wa mechi za hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, timu kutoka Kundi A, B, C na D ndio zilikuwa zinacheza mechi zake za tano na kila timu kubakisha mechi moja. Real Madrid ya Hispania ililazimika kusafiri hadi Ukraine kupambana na Shakhtar Donetsk.
Real Madrid ambao walishuka dimbani wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kipigo cha goli 4-0 kutoka kwa wapinzani wao wa jadi FC Barcelona, walianza kwa kasi ilikuweza kupata matokeo mazuri na kurudisha furaha yao katika vyumba vya kubadilishia nguo, jitihada za Real Madrid zilizaa matunda dakika 18 za kwanza baada ya Cristiano Ronaldo kupachika goli la kwanza.
Hadi dakika ya 70 Real Madrid walikuwa mbele kwa goli 4-0 kwa magoli ya Luka Modric dakika ya 50, Daniel Carvajal dakika ya 52 na Cristiano Ronaldo akapachika goli la nne dakika ya 70, Real Madrid walianza kujisahau na dakika ya 78 Shakhtar Donetsk wakapata goli la kwanza kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Alex Teixeira.
Shakhtar Donetsk waliendelea kujiamini na kufanya mashambulizi ambayo yalikuwa na madhara kwa Real Madrid, kwani dakika ya 83 Dentinho alipachika goli la pili na Alex Teixeira kwa mara nyingine tena dakika ya 89 akapachika goli la tatu na kufanya mchezo umalizike kwa Real Madrid kuibuka na ushindi wa goli 4-3 dhidi ya Shakhtar Donetsk. Kitu ambacho kinatajwa kama kungekuwa na muda wa ziada Shakhtar wangeweza sawazisha.
Matokeo ya mechi nyingine za UEFA zilizochezwa November 25
Kundi A
-
Malmoe FF 0 – 5 Paris Saint Germain
-
Shakhtar Donetsk 3 – 4 Real Madrid
Kundi B
-
CSKA Moscow 0 – 2 Wolfsburg
-
Manchester United 0 – 0 PSV Eindhoven
Kundi C
-
FC Astana 2 – 2 Benfica
-
Atletico Madrid 2 – 0 Galatasaray
Kundi D
-
Borussia Moenchengladbach 4 – 2 Sevilla
-
Juventus 1 – 0 Manchester City
Video ya magoli ya Shakhtar Donetsk Vs Real Madrid
https://youtu.be/khaSZJIjLn8
Video ya magoli ya Juventus Vs Manchester City
https://youtu.be/Et-fOlAqqek
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.