Kwenye headlines za dunia kipindi hiki huwezi kuacha kuzitaja headlines za Kiongozi wa Dini ya Kikatoliki duniani, Papa Francis kufanya ziara yake nchi za Afrika.. kwa sasa Papa Francis yupo Kenya kwa ajili ya ziara yake nchini humo huku mapokezi yake yakiweka headlines kwenye vituo mbalimbali vya habari duniani ikiwemo kituo cha Fox News, Marekani.
Nimetembelea mtandao wa kijamii wa Twitter na huko nimekutana na tweets nyingi sana za mashambulizi kutoka kwa Wakenya wakilaani kauli iliyoripotiwa na kituo cha habari Marekani, Fox News kilichosema ‘Pope visists War-Torn Africa’ kauli iliyowakwaza Wakenya wengi.
Wakenya wameona waongee waweke mambo sawa kwa kukiambia kituo cha Fox News kuwa hawana vita, wana amani na waache kuripoti taarifa zisizo sahihi… kama kawaida ripota wako nilichukua time ya kuzinasa tweets za wale wote waliochukua time na kuwaandikia Fox News hisia zao na kusisogeza kwako hapa chini kwenye hii post…
>>> “#SomeoneTellFoxNews mara ya mwisho kuwa na vita, ilikuwa kwenye twitter na CNN. Mkurugenzi wao ilibidi aombe msamaha kwa Rais wetu @UKenyatta.” <<< @WaturiWaMatu.
>>> “@SokoAnalyst @FoxNews Fox News, ongeleeni ujinga wa Wamarekani. Hakuna vita Africa! Siku hizi ni hatari zaidi kuishi nchi za nje! Jinga!” <<< @KavirondoGulf.
>>> “#SomeTellFoxNews watoto wa USA wanabeba bunduki kwenda nazo shule na kuua wanafunzi wenzao… sasa hawa tuwaite magaidi ama wanajeshi watoto?” <<< @OmarBond.
>>> “Kwanini tunagombana, #SomeoneTellFoxNews kwani hatujui kuwa @FoxNews ni habari takataka?” <<< @NaomiMutua.
>>> “#SomeoneTellFox tunajua mnataka muwe na trend dunia nzima, lakini kipaumbele hasi kama hiki kinamfaa Kim Kardashian na sio chombo cha habari@FoxNews” <<< @IsaacKegari.
>>> “Sijawahi kuisikia @FoxNews leo ndio mara ya kwanza. Hiki ni kipindi cha wanyama kinachoripoti kuhusu Mbweha, yani ni kitu kama documentary ama nini? #SomeoneTellFoxNews“. <<< @VictorMochere.
>>> “Hawa wajinga @FoxNews ni wepesi kuripoti takataka kuhusu Africa lakini hawawezi kuripoti kuhusu vurugu za matumizi ya bunduki US. #SomeoneTellFoxNews” <<< @VictorMochere.
>>> “#SomeoneTellFoxNews nyie ni wajinga kama watazamaji wenu wanaoamini ujinga wote mnaoripoti. Inueni miili yenu, fanyeni research na elimisheni umma wenu.” <<< @Nyarkogelo.
>>> “#SomeoneTellNewsFox hakuna sehemu nyingine ambayo tungependa kuwepo #LiveandDieinAfrika“. <<< @SautiSol.
>>> “Hizi media za nchi za nje zitajifunza lini? #SomeoneTellFoxNews“. <<< @CynthiaNyamai.
>>> “@FoxNews ujinga ni gharama. Wafundishe maripota wenu jiografia. Kenya haijaharibiwa na vita. Nendeni Syria. #SomeoneTellFoxNews“. <<< @Ben.
>>> “#SomeoneTellFoxNews watuombe msamaha kwa uzembe wa utoaji huu wa taarifa @foxnews“. <<< @Eric.
>>> “#SomeoneTellFoxNews Kenya sio C.A.R. Kenya ina amani kushinda Ufaransa na Chicago kwa ujumla“. <<< @Mlokole.
>>>”#SomeoneTellFoxNews kuwa #CNNWalijaribuNaWakafeli propaganda za kijinga. #KenyaIsMagical #TembeaKenya“. <<< @AhmedMohamed.
>> “#SomeoneTellFoxNews Kenya ina amani“. <<< @Mr.Onyancha.
Hii sio mara ya kwanza Kenya kuripotiwa vibaya na ikihusishwa na vita na ugaidi, kama unakumbuka CNN iliwahi kuandika kuwa Kenya ni ukanda wa ugaidi, Boss wa CNN akatua Kenya August 13 2015 kuonana na Rais Kenyatta kuomba radhi.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE