Jana klabu ya Manchester City ilikubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Juventus ikiwa ni ligi ya mabingwa Ulaya.
Kiungo wa Juve Paul Pogba jana usiku alionesha uzalendo kwa taifa lake hilo baada ya kuvalia viatu maalumu vyenye rangi ya bendera ya Ufaransa kama sehemu ya kuwaenzi wahanga wa shambulio la kigaidi lililotokea katika jiji la Paris, Ufaransa.
Kiungo huyo alikuwa mmoja wa watu waliokuwepo uwanjani wakati magaidi wanafanya mashambulizi nje ya uwanja wa Stade de France wiki iliyopita huku watu wasiopungua 124 wakipoteza maisha.
Baada ya ushindi huo, Juve imejikita kileleni mwa kundi D na kuiacha City katika nafasi ya 2 kila timu ikibakiwa na mchezo mmoja mkononi katika hatua ya makundi.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE