Rapper aliyekuwa anaunda kundi la muziki la G Unit, The Game aliingia kwenye headlines siku chache zilizopita baada ya kupost picha akiwa nusu mtupu kwenye page yake ya Instagram, lakini kwa muonekano wa mambo huenda kitendo cha rapper huyo kupost picha hizo kitamuingiza matatani na kampuni ya Instagram.
Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa picha mbili za awali zilizopostiwa na The Game zilipata malalamiko mengi kitendo kilichowashitua Instagram na kumuonya kuwa kitendo hicho kitamuingiza matatani ikiwa kumuweka kwenye danger zone ya kufutiwa account yake.
The Game ameonekana kutokujali onyo alilopewa badala yake aliendelea kupost picha hizo kwa madai ya kuwa anasaidia kuendesha soko la wauzaji boxers za kiume… na ukitembelea instagram page yake @losangelesconfidential sasa hivi bado utakutana na hizo posts kwenye timeline yake!
Hizi ni baadhi ya picha alizopost The Game, posts ambazo Instagram wametaka aache kuendelea kuziweka..
The Game alianza kwa kupost picha hii mwezi mmoja uliopita na caption ya maneno iliyosema…>>>”Tuseme leo nimedhani ni Ijumaa au #ThroughThatAZZbackThursday #WhoCaresWhatDayItis nasema leo ni #FineNiggaFriday kwa sababu najua utalike hii picha mpaka kesho…” <<< @losangelesconfidential.
Baada ya wiki moja kupita The Game akapost tena picha nyingine kwenye Instagram na maneno yaliyosema… >>> “kama mimi sio #ManCrushMonday wako basi atakuwa nani? … “<<< @losangelesconfidential.
Siku chache badaaye, The Game akapewa onyo lakini badala ya kuacha kupost picha hizi rapper huyo alipost picha nyingine na caption iliyosema… >>> “ahahaha, basi sawaa tuuze boxers basi…“<<< @losangelesconfidential.
Hii ilikuwa picha ya mwisho ya The Game kupost, lakini hatujui kama onyo la Instagram limemuingia ila kutokana na majibu anayotoa pale anapouliza, tutegemee chochote kutoka kwa rapper huyo!
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE