Jumapili ya November 29 klabu ya Arsenal itashuka dimbani kucheza mchezo wake wa Ligi Kuu Uingereza dhidi ya Norwich City katika uwanja wa Carrow Road, huu utakuwa mchezo wa 14 kwa Arsenal, Arsenal ambao watacheza mchezo wao November 29 mjini Norwich wamesafiri leo November 28 kuelekea huko ila safari yao imeingia katika headlines.
Arsenal ambao wameamua kusafiri kwa kutumia ndege binafsi kutoka London kwenda Norwich wameingia katika mzozo na watu wa mazingira kutokana na kusafiri kwa kutumia ndege ambayo imetumia dakika 14 hivyo wanadaiwa kuchafua mazingira, kwani safari ya umbali mfupi wangeweza kutumia usafiri wa basi.
Hata hivyo kocha wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amejitetea na kujibu kuwa wameamua kutumia usafiri wa ndege kutokana na barabara kuwa katika matengenezo, hivyo kama wangetumia usafiri wa basi wangekaa sana njiani, ndio maana wamefanya hivyo kukwepa msongamano. Hii sio mara ya kwanza kwa Arsenal kuingia katika mzozo na watu wa mazingira kwa kosa kama hilo, kwani waliwahi kuingia katika headlines hiyo mwaka 2012 baada ya kusafiri umbali wa maili 100 kwa kutumia ndege binafsi.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.