Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo.
Najua huenda stori nyingine zinakupita, hapa nimezikusanya zote zilizoguswa na #Tweets za #Magazeti November 29, 2015, unazisoma zote kwa pamoja.
Jeshi la Polisi Ruvuma linamshikilia mwanaume mmoja kwa kumuua mkewe na watoto wawili kwa kuwakata mapanga kisa wivu wa mapenzi #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amewasifu mashahidi wa Uganda kwa kuchagua kupoteza uhai wao ili kutetea imani #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
Maofisa watano TRA wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa agizo la Waziri mkuu ili kusaidia upelelezi wa upotevu wa makontena #MTANZANIA #NOV29

Mfanyabishara bilionea Mohammed Dewji ameshida tuzo ya mtu wa mwaka Afrika inayotolewa na jarida maarufu la Forbes #MTANZANIA #NOV29
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
Waziri mkuu wa zamani LOWASSA amekasirishwa na kushindwa kwa jeshi la Polisi kudhibiti vitendo vya kikatili dhidi ya raia #MTANZANIA #NOV29
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa JNIA amesema kuna watu wasio waaminifu ambao wanasafirisha nyara za Serikali kama ‘mboga’ #MTANZANIA #NOV29

Jeshi la Polisi Mara linamshikilia ofisa Utumishi mwandamizi kwa tuhuma za kuwalawiti watoto watatu wa kiume akiwa nyumbani kwake #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
Raia wawili wa Msumbiji waliokamatwa na pembe za faru Mbeya zenye thamani ya zaidi ya mil.82 wamehukumiwa jela miaka nane #MTANZANIA #NOV29
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
Mkazi wa Arusha amehukumiwa jela miezi 6 kwa kosa la kumtukana mwenzake kuwa ni mgumba, hana kizazi na alichonacho hakina faida #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
Wakazi wa Mpanda wamedaiwa kulazimika kuoa wake wengi ili kupata nguvu kazi itakayowasaidia wakati wa msimu wa kilimo #NIPASHE #NOV29
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
Mtoto wa marehemu Alphonce Mawazo amesema ndoto zake kuwa mwanasiasa zipo pale pale na waliomuua baba yake hawajakatisha ndoto yake #NIPASHE
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
Imeelezwa kesi nyingi zinazoripotiwa ktk madawati ya jinsia zinawahusu wanaume kunyanyaswa ikiwemo kupigwa na kubambikiwa watoto #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
Mtoto wa miaka mitano Kigoma amenajisiwa hadi kufa na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwao Kibondo, walimkuta peke yake #MZALENDO #NOV29
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
RC Dar ametangaza kiama kwa wakazi wa jiji hilo waliojenga katika bonde la mto msimbazi, operesheni ya Bomoabomoa itawakumba #MZALENDO NOV29
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
Rais mstaafu MKAPA amewataka Watanzania kumkumbuka kwa dhati rais aliyepita JK kwa uamuzi wake wa kujenga chuo kikuu cha UDOM #MZALENDO #NOV
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
Vichwa vitatu vya treni ambavyo vilinunuliwa na Serikali kwa takribani Sh. bilioni 15 vimetelekezwa licha ya kuhitajika #MZALENDO NOV29
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
M’kiti wa CHADEMA, MBOWE jana aliomba kibali kwa waombolezaji cha kumfungulia kesi RPC wa Mwanza kwa kuzuia MAWAZO kuagwa #TzDAIMA #NOV29
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
Wanaume wanaokumbwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye familia zao wametakiwa kuacha uoga na kwenda kutoa taarifa Polisi #TzDAIMA NOV
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
Utawala wa Rais MAGUFULI umeanza kupata misukosuko baada ya kupata upinzani kutoka kwa vigogo wa CCM wanaoathirika na utendaji wake #TzDAIMA
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
Serikali yataka vigogo wajipime kuhusu matumizi ya hovyo ya fedha za umma, kila mmoja anapaswa kujihoji akitembelewa atapona? #HabariLEO NOV
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
Wazee wanaoishi Bukoba vijijini wanalazimika kulala katika bweni moja wanaume na wanawake baada ya majengo kuezuliwa na upepo #HabariLEO NOV
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
Wananchi wamehamasishwa kujitokeza kusaidia kutoa ushirikiano kwa uongozi wa Rais MAGUFULI kuonyesha mali za vigogo wa TRA #HabariLEO #NOV29
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani kimeagiza kukamatwa mabasi yanayokiuka utaratibu kwa kupandisha nauli kiholela #HabariLEO NOV
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
Walimu zaidi ya 100 Shule za msingi na Sekondari Sengerema wameandamana kwa Mkurugenzi kudai malimbikizo yao yanayofikia bil.1.1 #JamboLEO
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
Tanzania imetajwa kuwa ya 33 miongoni mwa nchi 50 duniani ambapo wakristo wanakabiliwa na mateso yanayotokana na imani yao #MsamariaMWEMA
— millard ayo (@millardayo) November 29, 2015
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.