Headlines zimerudi China..mamlaka ya hali ya hewa imetoa tahadhari kwa watu kutoka nje baada ya kutokea uchafuzi wa mazingira ulioukumba mji mkuu wa nchini hiyo Beijing.
Mji huo ambao umekuwa katika hali ya tahadhari tangu mwanzoni mwa mwaka huu unasemekana kukumbwa na wingu zito baada ya mkaa kuwashwa maeneo mbalimbali kukabiliana na baridi kali.
Serikali ya China imetoa amri ya kutotoka nje kwa mamilioni ya watu kwa nia ya kupunguza madhara hayo kwao kwa muda wa siku tatu tangu jana jumapili na hali hiyo inatarajiwa kuendelea hadi siku ya Jumatano.
Viwango vya uchafuzi katika mji huo ni mara 17 zaidi ya viwango vya usalama vinavyotolewa na shirika la afya duniani WHO.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.