December 1 hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Challenge 2015 iliendelea kwa timu ya taifa ya Rwanda ikiongozwa na mchezaji wa Dar Es Salaam Young African Haruna Niyonzima kucheza mchezo wao na timu ya taifa ya Kenya, ikiwa ni siku moja toka Kilimanjaro Stars itolewe na mwenyeji wa mashindano hayo Ethiopia kwa mikwaju ya penati.
December 1 imekuwa zamu ya timu ya taifa ya Kenya kuaga michuano hiyo kwa mikwaju ya penati baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare 0-0, kwa mujibu wa sheria ya mashindano hayo dakika 90 za michezo ya robo fainali ikimalizika bila kupata mshindi inapigwa mikwaju ya penati ili kupata mshindi.
Rwanda wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya penati 5-3, mikwaju ya penati ya Haruna Niyonzima, Tuyisenge na Kizimana ilisaidia Rwanda kutinga hatua ya robo fainli ya michuano hiyo, kwa matokeo hayo sasa rasmi Kenya ambao walikuwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo wamevuliwa ubingwa. Timu zilizofanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ni Ethiopia, Uganda, Sudan na Rwanda.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.