Uwanja wa Stamford Bridge ni moja ya viwanja maarufu duniani katika mchezo wa soka, huu uwanja unamilikiwa na vigogo wa soka Chelsea.
Uongozi wa klabu hiyo tayari umewasilisha maombi ya mpango wake wa kupanua uwanja wao ili uweze kuingiza mashabiki 60,000 kwa wakati mmoja.
Pamoja na maombi hayo tayari manispaa ya London Borough of Hammersmith na Fulham imekaribisha maoni toka kwa wananchi ili watoe ridhaa yao au pingamizi kabla ya kuruhusu upanuzi wa uwanja huo ambao utalazimu kubomoa baadhi ya majengo yaliyo karibu na uwanja huo.
Chelsea, walianza kutumia uwanja wa Stamford Bridge, tangu 1905 ambapo mara ya mwisho kukarabatiwa na kupanuliwa ilikua mwaka 1990 na kuufanya uwe na uwezo wa kuchukua watazamaji 42,000.
Endapo ujenzi huo utaanza utamalizika mwaka 202o na utatumia kiasi ya Euro milioni 600.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.