Ikiwa bado siku moja Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli atimize mwezi mmoja toka aapishwe kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, tumeshuhudia mengi yakitokea katika suala zima la upambanaji na watu wanaokwepa kodi sambamba na kusimamishwa kazi kwa viongozi kadhaa wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) waliopo Bandarini.
December 4 kasi ya Rais John Pombe Magufuli inaonekana kuwashitua viongozi wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), kwani wameanza harakati za kuwaadhibu watu wanaodaiwa kodi, November 4 stori za kuaminika kutoka TRA ambazo zimeripotiwa na muhandishi wa habari za michezo Shaffih Dauda, zinatajwa kuizuia account ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), kwa kushindwa kulipa kodi ya Tsh bilioni 1.6.
Kitendo cha mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kuizuia account ya shirikisho la soka Tanzania (TFF), kinatajwa kuhusishwa na kasi ya Rais mpya wa awamu ya tano ambaye kwa kipindi hiki anaonekana kusimamia kila shilingi inayotoka na kuingia mahali fulani iwe imefuata utaratibu fulani sambamba na kuilipia kodi.
Msisitizo wake mkubwa Rais Magufuli katika suala la kodi ili wananchi wapate huduma “Kwa wale ambao bahati mbaya walikwepa kulipa kodi na wakayapitisha makontena, wasihangaike kuyafichaficha natoa siku saba tu wakalipe kodi halafu wakaishi kwa raha, kontena sio kama sindano ukilibeba mwishowe litakuponda bure“
Kama ulipitwa na msisitizo wa Rais Magufuli kuhusu kodi alivyoongea na wafanyabiashara kuhusu kodi video yake hii hapa.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.