Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo.
Najua huenda stori nyingine zinakupita, hapa nimezikusanya zote zilizoguswa na #Tweets za #Magazeti Desemba 06, 2015, unazisoma zote kwa pamoja.
Zaidi ya watu 100 waliokuwa wakisafiri kwa treni ya TRL kutoka Dar – Kigoma wamekwama Dodoma baada ya treni ya mizigo kuanguka #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
DAWASCO yapandisha bei ya maji kuanzia mwezi huu, wananchi waihadharisha kuhusu huduma bora na si ubabaishaji #MWANANCHI #DEC6 — millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Tume ya kudhibiti dawa za kulevya yavunjwa na inatarajiwa kuundwa nyingine,sasa faini ya watakaokamatwa ni bil.1 au jela miaka 30 #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Hospitali ya Amana imeanza kutoa huduma zake kwa njia ya mtandao ili kudhibiti upotevu wa mapato na kuboresha huduma #MWANANCHI #DEC6 — millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Manispaa za jiji la Dar zimetumia sh.bilioni 6 kwa ajili ya kufanya usafi katika kipindi cha mwaka wa fedha 2014/15 #MWANANCHI #DEC6
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Rais wa awamu ya nne JK ameibukia kwenye mkutano wa tano wa wakuu wa nchi za Afrika na China unaofanyika A.Kusini #MWANANCHI #DEC6 — millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Serikali imebomoa nyumba 150 huku nyingine zaidi ya 150 zikitarajiwa kuvunjwa baada ya kujengwa katika msitu wa hifadhi Morogoro #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Wakazi wa B’moyo wamemuomba Rais MAGUFULI kufuta hati za baadhi ya watu waliochukua ardhi zaidi ya eka 500 na kuitelekeza #MWANANCHI #DEC6 — millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Chuo kikuu cha Ushirika Moshi kimemuomba Rais MAGUFULI na Serikali yake kuwashughulikia watu wote wanaofuja mali za wana ushirika #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Watoto 150 wanaoishi na VVU Biharamulo wanakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi inayotishia kuzorotesha afya zao #MWANANCHI #DEC6 — millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Waziri wa ulinzi Marekani ametangaza kuwa nafasi zote za kazi za kijeshi na kivita sasa zitakuwa wazi kwa wanawake wa nchi hiyo #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Kocha wa Arsenal amesema mshambuliaji Alexis Sanchez alinusurika kifo J’pili baada ya kuanguka vibaya kwenye eneo la wapigapicha #MWANANCHI — millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Timu ya Uganda imethibitisha ubora wake baada ya kutwaa kombe la michuano ya Chalenji 2015, taji hilo lilikuwa Kenya mwaka jana #MWANANACHI
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Aliyekuwa kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar Alfred TIBAIGANA amesema Rais MAGUFULI amepatikana wakati sahihi #MWANANCHI #DEC6 — millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Rais KAGAME wa Rwanda azidi kubanwa kuwania tena Urais, mataifa ya Magharibi yataka aachie madaraka ifikapo mwaka 2017 #MWANANCHI #DEC06
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Watu waliokamatwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na makontena bandarini wafikia 47, miongoni mwao ni wafanyakazi wa TRA #NIPASHE #DEC06 — millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Mtoto wa miezi mitano ameibiwa Dar wakati akiwa msibani na mama yake, adai alimwachia msichana aliyekuwa jirani naye amwangalizie #NIPASHE
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Mtoto wa miezi mitano ameibiwa Dar wakati akiwa msibani na mama yake, adai alimwachia msichana aliyekuwa jirani naye amwangalizie #NIPASHE — millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
SUMATRA imefanya ukaguzi wa kushtukiza wa kupima ulevi madereva wa mabasi ya abiria yaendayo Mikoani na kubaini ulevi umepungua #NIPASHE DEC
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Raia wa Kenya anayekabiliwa na kesi ya dawa za kulevya ameiduwaza mahakama kuu Moshi baada ya kudai hafahamu kilichomfikisha hapo #NIPASHE — millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Serikali imeridhia ombi la kuanza ujenzi wa nyumba mpya 9,500 za askari wa Magereza pamoja na ununuzi wa magari kwa ajili yao #NIPASHE DEC06
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Siku 31 zimepita tangu Rais MAGUFULI aingie madarakani, usiri umeendelea kutanda juu ya lini atatangaza baraza lake la Mawaziri #NIPASHE DEC — millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Manispaa ya Temeke imetumia zaidi ya milioni 600 kuwahudumia na kuwatibu wagonjwa wa Kipindupindu tangu ugonjwa huo ulipoanza #NIPASHE DEC06
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Mtandao wa TGNP umeitaka Serikali kufanyia marekebisho sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kwa madai inaendeleza ukatili kwa watoto wa kik #NIPASHE — millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Mkoa wa Shiyanga ni miongoni mwa Mikoa ambayo wasichana wengi zaidi hukatizwa masomo kutokana na mimba za utotoni #NIPASHE #DEC06
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Kasi ya Rais MAGUFULI imeanza kuwatia matatani Marais wa nchi za A.Mashariki kwa wapigakura wao kutokana na uchapakazi wake #MTANZANIA DEC06 — millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Serikali imeshauriwa kuelekeza nguvu za mikopo ya elimu ya juu katika mtaji kwa wanafunzi wa vyuo vya ufundi stadi #NIPASHE #DEC06
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Maambukizi ya VVU Sengerema yamepungua kutoka 8.3% kwa mwaka 2005 hadi kufikia 2.6% mwaka 2015 #MTANZANIA #DEC06 https://t.co/TdZ5xF1GAZ — millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
51.9% ya watoto Kagera wanakabiliwa na utapiamlo kutokana na jamii kula aina moja ya mlo kila siku bila kuubadili #MTANZANIA #DEC06
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Raia wa Uganda wamekusudia kumpandisha kizimbani Rais wao MUSEVEN kupinga ukatili na unyanyasaji unaofanywa na Serikali yake #MTANZANIA DEC6 — millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Mkuu wa Mkoa wa Tanga MAHIZA amewasimamisha watumishi watano wa Idara ya Ardhi ili kupisha uchunguzi wa tuhumu zinazowakabili #MTANZANIA DEC
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Nyumba za walimu na Maabara ya shule ya Sekondari Hampangala iliyopo Mbeya imeezuliwa na upepo ulioambatana na mvua ya mawe #MTANZANIA DEC06 — millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Rais MAGUFULI ameiteka dunia kwa kuwa gumzo kila kona kutokana na uchapakazi, kukabiliana na watendaji wanaohujumu mali za umma #JamboLEO
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Maaskofu mbalimbali nchini wamepongeza utendaji kazi wa Rais MAGUFULI huku wakiimiza waumini kumwombea kiongozi huyo #GazetiUPENDO #DEC06
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Mchungaji Tb Joshua huenda akakamatwa kwa kushindwa kuhudhuria kesi inayomkabili ya vifo vya watu 116 iliyotokea kanisani kwake#GazetiUPENDO

Imeelezwa kuwa wanawake katika Manispaa ya Ilala wanaongoza kwa kuwapiga watoto wao na kuwafanyia vitendo vya ukatili #GazetiUPENDO #DEC06
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Mkurugenzi Tabora amevunja mikataba yote ya ujenzi iliyokuwa inatekelezwa na kampuni ya Saram kwa kushindwa kutekeleza majukumu #JamboLEO

Tanzania imetangazwa rasmi kuwa ni mojawapo ya nchi isiyokuwa na ugonjwa wa Polio ktk nchi za Afrika #MZALENDO DEC06 https://t.co/TdZ5xF1GAZ

Baadhi ya wanafunzi wa kike wanaosoma Sekondari Mkoani Rukwa wamejikuta wakiwekwa kinyumba baada ya wazazi/walezi kuwatelekeza #HabariLEO
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Serikali imesema idadi ya watumiaji wa huduma za simu imeongezeka kutoka milioni 2.96 mwaka 2005 hadi milioni 32.1 mwaka 2014 #HabariLEO DEC
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
TAMISEMI imeagiza watumishi wawili waandamizi Manispaa ya Morogoro kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa utendaji kazi wao #HabariLEO DEC06
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Nyati 8 wenye thamani ya milioni 32.6 wamekufa hapo hapo baada ya kugongwa na Fuso wakati wakivuka barabara eneo la Mikumi #HabariLEO #DEC06
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Wanawake wanaofanya biashara ya mamalishe wanaongoza kwa kufanyiwa vitendo vya ukatili katika masoko mbalimbali nchini #TzDAIMA #DEC06
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
TACAIDS imesema takwimu zinaonyesha vijana ambao ni wanafunzi wa vyuo mbalimbali wapo hatarini kupata maambukizi mapya ya VVU #TzDAIMA DEC06
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Utawala wa JK unadaiwa kuchelewesha utangazaji baraza la Mawaziri la Rais MAGUFULI ambaye amekuwa akitumia muda mwingi kutafakari #TzDAIMA
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Kamati kuu ya CCM inatarajia kufanya kikao kesho Dar chini ya M'kiti JK kujadiliwa na kupitisha majina ya makada watakaowania Umeya #TzDAIMA
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Mahakama ya Bunda imemuhukumu kifungo cha miaka 30 jela mzee wa miaka 54 kwa kosa la kumuoa na kumbaka mtoto wa miaka minne #TzDAIMA #DEC06
— millard ayo (@millardayo) December 6, 2015
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.