Licha ya kuwa mchezo wa soka unahitaji ubunifu maarifa na ufundi, kasi pia ni moja kati ya kitu kinachomuongezea thamani mchezaji, kuna baadhi ya namba uwanjani uhitaji wachezaji wenye kasi zaidi. Kama ambavyo kwa Tanzania Mrisho Ngassa anatajwa kuwa na kasi, kiasi hata cha mkenya McDonald Mariga kumsifia, ila wapo wachezaji wengine wanaotajwa kuwa na kasi zaidi duniani. Hadi kufikia mwezi May 2015 hii ndio ilikuwa Top 5 ya wachezaji soka wenye kasi zaidi duniani, stori kutoka talksport.com
5- Theo walcott ni moja kati ya mastaa wa soka wa Uingereza wenye kasi zaidi duniani, Walcott kwa mujibu wa talksport.com anatajwa kuwa na uwezo wa kukimbia Kilometa 32.7 kwa saa.
4- Staa wa soka wa klabu ya Real Madrid ya Hispania na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo anatajwa kuwa na uwezo wa kukimbia kwa kasi ya Kilometa 33.6 kwa saa. Uwezo ambao unamfanya aingie katika list ya mastaa watano wenye kasi zaidi duniani.
3- Aaron Lennon licha ya kuwa katika list ya wachezaji wafupi zaidi wanaocheza Ligi Kuu Uingereza Aaron Lennon yupo katika Top 5 ya mastaa wenye kasi zaidi uwanjani. Lennon anatajwa kuwa na uwezo wa kukimbia Kilometa 33.8 kwa saa.
2- Gareth Bale inatajwa ni nadra sana kumkosa staa huyu katika Top 5 hii, kwani amewahi kuingia katika headlines za kumzidi mbio moja kati ya mabeki bora duniani Maicon. Hivyo ni nadra sana kukosekana katika headlines za mastaa wenye kasi zaidi. Bale anatajwa kuwa na uwezo wa kukimbia kwa kasi ya Kilometa 34.7 kwa saa.
1- Antonio Valencia ni staa wa soka kutokea Ecuador, anatajwa kuwa na uwezo wa kucheza nafasi mbili kwa ufasaha uwanjani, kama winga wa kulia na beki wa kulia, Valencia ambaye anakipiga katika klabu ya Manchester United ya Uingereza anatajwa na mtandao wa talksport.com kuwa mchezaji kasi zaidi duniani, ana uwezo wa kukimbia kwa kasi ya Kilometa 35.1 kwa saa.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.