Shirikisho la soka Afrika (CAF) limesema Sierra Leone sasa iko huru kuwa mwenyeji wa mechi mbalimbali za kimataifa.
Awali CAF ililifungia Taifa hilo kuandaa michuano yoyote ya kimataifa kutokana na kukumbwa na ugonjwa wa Ebola ambao ulichukua headlines kwa kiasi kikubwa.
Nchi hiyo ya Afrika Magharibi ilipigwa marufuku kuandaa mechi zozote za kimataifa tangu mwaka 2014 kufuata ushauri wa shirika la afya duniani WHO baada ya kutokea kwa ugonjwa wa Ebola.
Watu zaidi ya 10,000 walipoteza maisha tangu Dissemba mwaka 2013 na wengine kutoka nchi za Liberia na Guinea.
Katika mataifa hayo matatu, ni Guinea pekee sasa ambayo hairuhusiwi kuandaa mechi za CAF, kwa kuwa bado haijatangazwa kuwa huru kutokana na ugonjwa wa Ebola.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE