Siku chache zilizopita wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha urafiki walifanya mgomo kwa madai ya kutolipwa mishahara yao kwa muda mrefu kupelekea mkuu wa wilaya ya Kinondoni, DC Paul Makonda kuagiza shughuli zote za kiwanda hicho zisimame mpaka mgogoro wa kimaslahi kati ya wafanyakazi na wamiliki wa kiwanda hicho utakapotatuliwa.
Sasa leo kupitia kwenye ukurasa wa instagram DC Paul Makonda aliandika maneno kuhusu namna alivyotatua mgogoro huo na kufanikisha kile kiasi wanachotakiwa kulipwa wafanyakazi kiwanda cha nguo cha URAFIKI kilichopo eneo la Shekilango Dar es Salaam.
‘Asante Mungu kwa kuniwezesha kuwatetea wanyonge wenzangu na wafanyakazi wa kiwanda cha urafiki na kufikia kulipwa kiwango 150000 tofauti na hapo zamani walipokuwa wanalipwa 80000 kwa mwezi….Jambo ambalo wameliomba tangu 2007′>>>>Paul Makonda
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokeamatukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayokwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.