Kama ilivyo ada mtu wangu imekuwa ni kawaida kwa watu mbalimbali kupost picha zao kwenye mitandao ya kijamii kama kumbukumbu ya kule walipotokea. Alhamisi imekuwa kama siku maalum ya kuweka hizo picha mitandaoni hasa katika mitandao ya Instagram, Facebook na Twitter.
Nimeamua kukusogezea baadhi ya Pichaz za mastaa wa soka ambao umezoea kuwaona wakiwa uwanjani na inawezekana ukawa haujawahi kuwashuhudia enzi zao za utotoni.
Edson Arantes do Nascimento ni jina lake kamili alilobatizwa na wazazi wake, najua wengi wenu mmemzoea kwa jina la Pele. Ni mchezaji bora wa muda wote kutoka Brazil, Staa huyo ameshachezea timu ya Santos iliyopo Brazil pamoja na New York Cosmos ya Marekani. Pele ameichezea pia timu ya taifa Brazil na kutwaa mataji matatu ya Kombe la Dunia.
Oscar wa Chelsea jina lake kamili anaitwa Oscar dos Santos Emboaba Júnior, amezaliwa nchini Brazil, ni kiungo wa kati kwenye klabu ya Chelsea hivi sasa na alianza maisha yake ya soka akiwa na Sao Paulo ya Brazil mwaka 2009.
Peter Cech amezaliwa Jamhuri ya Czech ambaye anacheza nafasi ya golikipa katika klabu ya Arsenal pamoja na timu ya Taifa ya Jamhuri ya Czech. Cech alishawahi kuitumikia klabu ya Chelsea ambayo alijiunga nayo mwaka 2013 na baada ya hapo akahamia Arsenal mwaka 2015.
Alexandre Pato ni mchezaji ambaye amezaliwa Brazil, kwa sasa anaitumikia klabu ya Corithians inayoshiriki Ligi Kuu ya Brazil. Pato ameshawahi kuzitumikia timu mbalimbali ikiwemo Sao Paulo iliyopo Brazil pamoja na AC Milan ya Italia. Pato ameshaitumikia pia timu yake ya taifa ya Brazil.
Diego Maradona ni Staa aliyestaafu kucheza soka, amezaliwa jijini Lanus Argentina, amezitumikia timu mbalimbali kama FC Barcelona, Bocca Juniors na amebahatika kuitumikia timu yake ya taifa ya Argentina. Waingereza wanamchukia mpaka leo hii mtu wangu kwa goli lake la mkono alilofunga dhidi ya Uingereza mwaka 1986 huko nchini Mexico.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.