Inawezekana ukawa na hamu ya kufahamu vitu vingi vinavyoendelea kwa sasa katika shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), sasa stori ninayotaka kukusogezea ni hii kuhusiana na miradi ya umeme inayoendelea nchini.
Akizungumza mkurugenzi wa Tanesco,Mhandisi Felchesmi Mramba Dec 14 alisema…’Miradi inayotekelezwa ni pamoja na ule unaojengwa kusnini mwa Dar es Salaam kwa mkopo wa Benki ya Dunia ambao utaboresha umeme maeneo ya Kigamboni, Kurasini, Kisarawe, Gongolamboto, Ukonga, Kitunda, Vingunguti na Tabata‘>>>Mramba
‘Mradi mwingine ni unaotekeleza kwa ufadhi wa Serikali ya Japan ambao utasaidia kuondoa matatizo yaliyo katika maeneo ya Muhimbili na Upanga, Mwananyamala na Kinondoni, Oysterbay na Masaki, Jangwani Beach, Bahari Beach na Mbezi Beach‘>>>Mramba
‘Sambamba na miradi hiyo inayotekelezwa Dar mradi mkubwa wa kupeleka umeme wa 400KV kutoka Iringa kupitia Mtera, Dodoma, Singida, hadi Shinyanga….uko kwenye hatua za mwisho za kukamilika na hivyo kutuhakikisha umeme wa uhakika katika kanda ya ziwa hasa jiji la Mwanza‘Mramba
‘Kazi za kuunga Tanzania na Kenya kwa umeme wa 400KV inatarajiwa kuanza hivi karibuni kwani kuwapata Makandarasi ziko katika hatua za mwisho….Ujenzi unategemea kuanza mwakani‘>>Mramba
‘Kazi nyingine ambazo hazijaanza lakini zitaanza hivi karibuni ni pamoja na Dar es Salaam -Somanga (400KV), Bulyankhulu- Geita – Nyakanazi – Rusumo (220KV)…miradi hii ya kuimarisha miundombinu ikikamilika itasaidia kupunguza kiasi kikubwa tatizo la kukatika kwa umeme kutokana na mfumo wa usambazaji‘>>>Mramba.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE