Baada ya dirisha la usajili la Ligi Kuu Uingereza kufungwa mara nyingi wachezaji wanaosajiliwa kwa dau kubwa huwa wanaingia katika headlines za kupanda kwa mishahara yao. Miongoni mwa wachezaji wapya walioingia katika list ya TOP 10 ya mastaa wanaolipwa mishahara mkubwa ni Raheem Sterling. Stori kutoka sokka.com hii ndio list ya mastaa wa soka wa Uingereza wanaolipwa mishahara mikubwa.
10- Nahodha wa klabu ya Chelsea John Terry yupo katika list analipwa pound 160000 kwa wiki.
=8- Kevin De Bruyne huyu ni moja kati ya sura mpya zilizojiunga na Man City msimu huu akitokea klabu ya VLF Wolfsburg ya Ujerumani. De Bruyne analipwa pound 170000.
8- Nyota wa zamani wa klabu ya Arsenal ya Uingereza ambaye anakipiga katika klabu ya Chelsea ya Uingereza Cesc Fabregas anavuta mshahara wa pound 170000 sawa na Kevin De Bruyne wa Man City.
7- Raheem Sterling kabla ya uhamisho wake wa pound milioni 49 kutoka Liverpool kujiunga na Man City hakuwa hata katika TOP 20 ya wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa, ila kwa sasa anavuta mshahara wa pound 180000 kutoka Man City..
6- Mfalme wa assist anayekipiga katika klabu ya Arsenal Mesut Ozil anatajwa na mtandao wa sokka.com kuwa analipwa na Arsenal mshahara wa pound 190000 kwa wiki mkwanja.
5- David Silva ambaye anatajwa kuwa ndio kiungo mbunifu katika Ligi Kuu Uingereza, anavuta mshahara wa pound 200000 kwa wiki ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 500 za kitanzania.
4- Eden Hazard alikuwa anawaniwa na klabu ya Man United kabla ya mwaka 2012 kuamua kujiunga na Chelsea. Hazard anavuta mkwanja wa pound 220000 kwa wiki.
=2- Yaya Toure huyu ndio staa pekee kutoka bara la Afrika anaolipwa mshahara mkubwa katika Ligi Kuu Uingereza analipwa pound 240000 kwa wiki, mshahara ambao ni sawa na mchezaji mwenzake wa Man City Sergio Aguero.
2- Sergio Aguero anakamilisha list ya wachezaji watano wa Man City wanaoongoza kwa kulipwa mkwanja mrefu anavuta mshahara wa pound 240000 sawa na Yaya Toure.
1- Wayne Rooney ndio staa wa kwanza anayelipwa mshahara mkubwa Ligi Kuu Uingereza. Rooney anavuta mkwanja wa pound 260000 akiwa na klabu ya Man United. Mshahara wa Rooney ni zaidi Tsh milioni 600 za kibongo kiwango ambacho ukizidisha mara wiki nne za mwezi mmoja unapata bilioni 2.4 za kibongo, huo ni mshahara wa Rooney wa mwezi ambao kwa makadirio ya kawaida bajeti ya vilabu vyote vya Ligi Kuu kiundeshaji wake kwa mwezi mmoja.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.