Leo viongozi wa CHADEMA wamekutaka na kuzungumza mambo mbalimbali mbele ya waandishi wa habari.
Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA Salum Mwalimu amezungumzia mchakato wa kuwapata Mameya watakaowakilisha Wilaya za Kinondoni na Ilala.
Upatikanaji wa Meya wa Ilala na Kinondoni wamejibu kuwa..“CCM inaendeleza falsafa yao ile ile ya kujiona wao wanaweza wakapindisha mambo kadri wawezavyo, leo ushahidi upo.. pale ambapo wanashinda Halmashauri tunawaacha waendelee na taratibu zao, lakini pale wanaposhinda UKAWA wanakuwa magumu kukubali matokeo, tunawaomba wakazi wa maeneo yote waliyoipa CHADEMA nafasi tutahakikisha tunasimamia ukweli”…Salum Mwalimu.
“Temeke leo tayari wamepata Meya, kwa sababu CCM walikuwa na madiwani wengi na sisi hatukuleta njama yoyote ya kutaka kuvuruga, lakini leo Ilala ambapo UKAWA ndipo wenye madiwani wengi Meya bado hajapatikana, hivyo hivyo na Kinondoni, huu ni mfano mdogo wa hapa hapa Dar es salam ukiachilia mbali Mikoani”…Salum Mwalimu
“Tunashukuru ndani ya chama tumemaliza kupata madiwani wanaowania nafasi ya Umeya kwa Ilala atakuwa Charles Kuyego na Kinondoni ni Boniface Jacob wote wanatoka CHADEMA..watakaopeperusha bendera ya UKAWA katika nafasi ya Umeya, tunajiamini kwa sababu tuna madiwani wengi ambao ndio wanakwenda kuchagua viongozi hawa, tunataka kuandika historia ndani ya miaka mitatu ijayo, uwezo upo, rasilimali ipo, kilichokosekana ni dhamira ya kweli“..Salum Mwalimu.
Meya atakayepeperusha bendera ya UKAWA wa jiji la Dar es salaam…”Ndugu Isa Mwita ndiye atakayegombea nafasi ya Umeya wa jiji la Dar es salaam ambaye ndiye mgombea pekee wa CHADEMA akiungwa mkono na UKAWA, tumejipanga kuwatumikia wakazi wa Dar es salaam kwa ukamilifu, changamoto zinazoikabili tunataka kuandika historia ndani ya miaka mitatu ziwe zimepungua ama zimemalizika”..Tunaomba tume ya Taifa ya uchaguzi imalize changamoto zote zilizosalia kwenye uteuzi wa madiwani wa viti maalum “.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.