Headlines za soka la kimataifa kwa sasa ni kuhusu uongozi wa klabu ya Chelsea kuamua kumuachisha kazi Jose Mourinho, taarifa ambazo zilitoka mchana wa December 17. Kila mtu kaongea lake ila AMPLIFAYA ya Clouds FM iliwatafuta wachambuzi na waandishi wa habari za michezo Edo Kumwembe na Saleh Ally kuhusu uamuzi wa Chelsea kumfuta kazi ni uamuzi sahihi kwa Chelsea kufanya hivyo?
“Kufukuzwa kwa Mourinho ni kitu ambacho kilikuwa kinatarajia kwani maboss tayari walikuwa wamechoka na matokeo mabovu, ukumbuke kuwa kipigo cha Leicester City kilikuwa cha tisa kwa Chelsea. Tatizo la Chelsea lilikuwa katika vyumba vya kubadilishia nguo, kwani aligombana na doctor Eva, Terry, Ivanovic na Costa kitu ambacho kilichangia matokeo mabovu” >>>> Edo Kumwembe
“Kwa mpira sahihi Abramovich alichelewa kumuondoa Mourinho, kwani kocha bora analindwa na matokeo ukilinganisha takwimu ya matokeo ya mechi zao 16, ukizungumzia tatizo la Mourinho kwa Chelsea halipo kiufundi kwa maana ufundishaji wake hauwezi kufeli kwa miezi sita, hivyo huenda wachezaji hawakuridhishwa na tabia kumuondoa Eva hivyo wameonesha hisia zao” >>> Saleh Ally
Hadi sasa klabu ya Chelsea iliyotangaza kumfuta kazi Jose Mourinho mchana wa December 17, ipo nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa imecheza jumla ya mechi 16, imeshinda mechi nne, kufungwa tisa na sare mechi tatu.
Hii ni sauti ya kwanza ya Edo Kumwembe na ya pili ya Saleh Ally unaweza sikiliza walichokisema kuhusu Mourinhoa
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.