December 23 2015 imenifikia taarifa ya maamuzi yaliyoamriwa na Serikali ya Tanzania ambapo Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Mabasi ya mwendokasi DART, Bi. Asteria Mlambo amesimamishwa ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.
Tuhuma zilizotajwa kusababisha kusimamishwa kwa Mkurugenzi huyo ni ishu ya kukiukwa kwa kanuni za kumtafuta mtoa huduma wa mpito wa huduma za mabasi ya mwendokasi.
Katika kukiukwa kwa kanuni hizo, Serikali imesema kuna watumishi ambao watachunguzwa na kuchukuliwa hatua kwa kushindwa kumshauri vizuri Mtendaji Mkuu huyo.
Taarifa hiyo kutoka kwa Waziri George Simbachawene hii hapa..
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.