Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea tena kwa michezo miwili kupigwa, Mwanza ulichezwa mchezo wa Toto Africans dhidi ya African Sports ya Tanga, wakati Dar Es Salaam katika dimba la Azam Complex Chamazi, kulikuwa kuna mchezo wa kuvutia kati ya Azam FC dhidi ya Kagera Sugar.
Azam FC ambao walikuwa katika uwanja wao wa nyumbai Azam Complex Mbande Chamazi waliikaribisha Kagera Sugar ya Kaitaba Bukoba, katika kucheza mchezo wao wa 12 wa Ligi. Mchezo ulikuwa wa kuvutia kwa upande wa timu zote mbili, licha ya kuwa Azam FC walipata goli la kwanza mapema dakika ya 11 ya mchezo kupitia kwa Kipre Tchetche.
Licha ya goli la mapema la Azam FC, Kagera Sugar walionekana kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa na kuwa shambulia Azam FC na kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza walipata penati, baada ya mchezaji wa Azam FC kushika mpira katika eneo la hatari na penati kupigwa na Salum Kanoni na kupanguliwa na golikipa wa Azam FC.
Azam FC walitumia mbinu ziada kuifunga Kagera Sugar ambayo ilikuwa inaonekana kumiliki mpira mara kwa mara na kukosa nafasi ila kipindi cha pili Azam FC walirudi kwa umakini mkubwa na dakika ya 78 beki wao wa kulia Shomari Kapombe na kuhitimisha ndoto za Kagera Sugar kutaka kusawazisha na kuambulia walau point mmoja.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.