Headlines kwenye vyombo vya habari zinabebwa na neno ‘jipu’ au ‘majipu’ kutokana na kauli na ahadi ya Rais Magufuli kwamba lazima atumbue majipu ya ufisadi na ubadhirifu Serikalini.
Tuliyapata ya upotevu wa makontena zaidi ya 2,000 bandarini ambayo yalitoroshwa bila kulipia ushuru, Serikali ikaamua baadhi ya watumishi wakamatwe na kesi zao zinaendelea Mahakamani… kingine kilichoripotiwa na gazeti la Mwananchi ni kuhusu bandarini hapohapo…
Waziri aliyeapishwa jana, Prof. Makame Mbarawa amesema Serikali imepoteza jumla ya bilioni 48.77 baada ya makontena 11,884 na magari 2,019 kupitishwa bandarini Dar bila kulipiwa ushuru.
Waziri Prof. Makame Mbarawa amesema watu saba wamekamatwa na wengine nane bado wanasakwa kwa kuhusika na tuhuma hizo.
Stori kutoka kwenye ukurasa wa gazetini >>> MWANANCHI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE