Baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Samatta kuthibitisha kuwa yuko mbioni kuondoka TP Mazembe na kujiunga na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, stori za January 2 ni kuwa klabu ya TP Mazembe imeita nyota wawali wa bongo kwenda kufanya majaribio.
TP Mazembe ambayo inachezewa na watanzania wawili Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu imeonekana kuanza kuvutiwa na huduma ya wachezaji kutoka Tanzania, hivyo imewaita kwa majaribio ya wiki mbili wachezaji wawili wa Stand United ya Shinyanga Haruna Chanongo na Abuu Ubwa.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Haruna Chanongo ameshawahi kuichezea klabu ya Simba kwa muda kidogo, kabla ya kuamua kwenda kulinda kipaji chake kwa kuichezea klabu ya Stand United. Wakati Abuu Ubwa amewahi kuichezea klabu ya Atletico Sport Clube Reguengos ya daraja la kwanza nchini Ureno.
CHANZO CHA STORI HII: Salehjembe.com
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.