Mshambuliaji wa kimataifa wa Mexico ambaye amewahi kuichezea klabu ya Man United kwa miaka kadhaa Javier Hernandez Chicharito kabla ya mwaka 2015 kuamua kujiunga na klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani, amekuwa akihusishwa kuhitajika na klabu ya Arsenal ya Uingereza.
January 3 mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Rudi Voller ameongelea uwezekano wa mchezaji huo kuondoka ndani ya Leverkusen ni mdogo sana hususani ukizingatia wapo katikati ya msimu, hivyo ni ngumu kwa wao kumuacha aondoke. Jibu hilo linakuwa pigo kwa Arsenal ambao wanatajwa kuwa walikuwa na imani ya kumpata.
“Chicharito ana nafasi kubwa sana ndani ya kikosi chetu, hususani kwa aina yake ya ushambuliaji na ndio maana tukamsajili katika timu yetu, ndio kwanza tupo katikati ya msimu na kila kitu kinaenda sawa ni rahisi kukataa ofa za vilabu vingine” >>> Rudi Voller
Kauli ya Rudi Voller inalenga kuvikatisha tamaa vilabu vya Ulaya ambavyo vimekuwa vikivutiwa na huduma ya mmexico huyo. Chicharito hadi sasa amefunga magoli 11 katika michezo 1 aliyocheza katika Ligi Kuu Ujerumani.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.