Kuna wakati Vyuo vikuu Tanzania ilibidi zianze kutangazwa na kupitishwa kanuni za mavazi ambayo wanafunzi wanatakiwa kuvaa, ule uhuru ulifanya wengine kuvaa mpaka nguo ambazo sio sahihi kuvaa hadharani !! Pata picha ni mgahawani na bado hauruhusiwi kuvaa nguo za aina fulani.
Mgahawa huo wa McDonald ulipo maeneo ya Oak Wood, Melbourne Australia waliweka tangazo la kwanza lililoandikwa hivi >’No shirts, No shoes, No service‘< ‘Kama hujavaa shati au viatu hakuna huduma‘.
Baadae ikaonekana tangazo hilo sio sawa, ni kama imetumika lugha kali hivi… likafatia tangazo jingine kuwaomba wateja wao wavae viatu na mashati >’For the comfort of all customers we request shirts and shoes to be worn when in store please‘<
Wamiliki wa mgahawa huo walifikia hatua hiyo baada ya wateja wengi kuwa na tabia ya kufika kwenye mgahawa huo wakiwa wamevaa nguo za kuogelea kutoka kwenye bwawa lililo jirani, wakati mwingine wanakuja na majimaji ambayo yanasababisha utelezi kwenye mgahawa huo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.