Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayeichezea klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo amefanikiwa kuweka rekodi kadhaa kubwa katika soka, ukiachana na kutwaa tuzo ya tatu ya mchezaji bora wa Dunia Ballon d’Or kwa mwaka 2015, Ronaldo amefanikiwa kuweka rekodi 7 mpya.
7- Ronaldo amefanikiwa kufunga jumla ya hat-trick 28 katika kipindi cha mwaka 2009-2015, toka amejiunga na Real Madrid mwaka 2009 hadi 2015, Ronaldo anakuwa mchezaji anayeongoza kwa ufungaji wa hat-trick nyingi katika historia ya Laliga.
6- Kufunga magoli 48 kwa msimu mmoja akiwa na Real Madrid. Ronaldo alifunga jumla ya magoli 48 katika msimu wa 2014/2015 na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli mengi katika msimu ndani ya Real Madrid.
5- Kufunga magoli 50 kwa misimu mitano mfululizo. Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza Hispania kufunga magoli 50 katika misimu mitano mfululizo, alianza kufanya hivyo mwaka (2010/11–2014/15).
4- Kufunga magoli 61 kwa msimu mmoja katika mashindano yote aliyocheza ndani ya msimu wa mwaka 2014/2015.
3- Kuvunja rekodi ya ufungaji wa goli 323 ya mkongwe wa Real Madrid Raul. Ronaldo amefunga jumla ya 338 hadi sasa katika michezo 325 ndani ya Real Madrid, wakati Raul aliweka rekodi ya kufunga goli 323 kwa kucheza michezo 741.
2- Kuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli 11 katika michuano ya klabu Bingwa Ulaya hatua za makundi kwa msimu wa 2015/2016.
1- Kuwa mchezaji pekee kutwaa tuzo ya mfungaji bora wa Ulaya mara nne kwa kufunga jumla ya goli 48 kwa msimu wa 2014/2015.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.