Kamati ya maadili ya FIFA imependekeza katibu mkuu wa shirikisho hilo linalosimamia soka duniani Jerome Valcke asimamishwe kujihusisha na mchezo wa soka kwa miaka tisa.
Katibu huyo anadaiwa kutumia vibaya pesa ikiwemo uuzaji wa tiketi za kombe la duniani lililopita pamoja na kukiuka sheria za Shirikisho hilo.
Awali kamati ya nidhamu alimsimamisha katibu huyo kwa siku 90 kutojihusisha na mchezo wa soka ambapo adhabu yake imemalizika leo lakini ameongezewa adhabu kwa siku nyingine 45 wakati uchunguzi ukiendelea.
Jerome ataungana na viongozi wengine Sepp Blatter aliyekuwa Rais wa FIFA pamoja na makamu wake Michel Platini ambao wote wamesimamishwa tangu mwezi uliopita kwa miaka nane baada ya uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha kukamilika.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.