Bado hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar inazidi kushika kasi kila kukicha, baada ya mchana wa January 6 kupigwa mchezo wa tatu wa Kundi A lenye timu za URA, JKU, Jamuhuri na Simba, usiku wa January 6 ukapigwa mchezo wa nne wa kundi hilo kwa kuzikutanisha timu za URA ya Uganda dhidi ya Simba.
Simba ambao mchezo wa kwanza walitoa sare ya kufungana goli 2-2 dhidi ya Jamuhuri waligoma kurudia makosa na leo January 6 wakaiadhibu URA ya Uganda kwa kipigo cha goli 1-0, goli ambalo pasi yake ilipikwa vizuri na Mwinyi Kazimoto dakika ya 37 kipindi cha kwanza na Ibrahim Ajib akapachika goli kwa shuti kali.
Kwa matokeo hayo Simba sasa itakuwa inaongoza Kundi B, ikiwa na point nne, ikifuatiwa na URA ya Uganda wenye point tatu sawa na JKU ya Zanzibar ila URA anakuwa mbele ya JKU kwa tofauti ya magoli. wakati Jamuhuri ikishika mkiwa kwa kuwa na point moja pekee.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE