Michuano ya Kombe la Mapinduzi January 7 imeendelea kwa mchezo wa tano wa Kundi B kupigwa wakati mwingine ukitarajiwa kupigwa usiku wa January 7. Mchezo wa tano wa kundi B ulichezwa kwa kuzikutanisha timu za Azam FC dhidi ya timu ya Mafunzo inayomilikiwa na jeshi la magereza.
Mchezo wa Azam FC dhidi ya Mafunzo ulipigwa katika uwanja wa Amaan na Azam FC kukubali kipigo cha goli 2-1, licha ya kuwa Azam FC ndio walikuwa wa kwanza kufunga goli la kuongoza kupitia kwa Kipre Tchetche dakika ya 20 kipindi cha kwanza na kuweka matumaini ya Azam FC kusonga mbele katika hatua inayofuata.
Matumaini ya maisha ya Azam FC kuendelea kusalia katika michuano ya Kombe la Mapinduzi yalianza kupotea dakika ya 35 kipindi cha kwanza baada ya Mafunzo FC A.K.A wajelajela walisawazisha goli kupitia kwa Rashid Abdallah ila Mafunzo walithibitisha safari ya Azam FC kurudi Dar Es Salaam dakika ya 90 baada ya Rajab kupachika goli la ushindi kwa Mafunzo.
Kwa matokeo hayo mchezo kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga utakaochezwa saa 20:15 utakuwa wakukamilisha ratiba, kwani Mafunzo na Azam FC wote wametolewa mashindanoni, Yanga na Mtibwa Sugar ambao kila mmoja ana point nne watacheza mchezo wa kutafuta nani apate nafasi ya kuongoza Kundi B. Hii ni mara ya kwanza kwa Azam FC kutolewa katika Kombe la Mapinduzi katika hatua za Makundi.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE