Mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon anayekipiga katika klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani Pierre-Emerick Aubameyang ameingia kwenye headlines usiku wa January 7, baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa mwaka 2015. Aubameyang ameshinda tuzo hiyo kwa kuwazidi kura Andrew Ayew na Yaya Toure.
Baada ya ushindi huo Aubameyang akaulizwa maswali kuhusu kuhusishwa kwa kiasi kikubwa na mpango wa kujiunga na klabu ya Arsenal ya Uingereza. Staa huyo wa Borussia Dortmund aliwahi kukiri kuwa na mipango ya kucheza soka Ligi Kuu Hispania.
Aubameyang amejibu hivi kuhusu stori za yeye kujiunga na klabu ya Arsenal “Naomba niseme kitu kimoja sina mpango wa kujiunga na Arsenal, Dortmund ndio klabu yangu na sifikirii kuhama hivi karibuni. Siku zote mimi sio mchezaji wa kutekwa na hisia za kulia ila kushinda tuzo hii mbele ya Toure na Ayew imefanya nilie” >>> Aubameyang
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.