Klabu ya soka ya Chelsea ambayo ilikuwa na matumaini kwa kiasi kikubwa kupata saini ya moja kati ya wachezaji wa kibrazil, January 19 imekataliwa kuuziwa mchezaji na klabu inayo mmiliki. Chelsea ambayo kwa sasa ipo na kocha wa muda Guus Hiddink ilikuwa inahitaji kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayeichezea klabu ya Shakhtar Donetsk Alex Teixeira.
Chelsea walikuwa wanatajwa kwa karibu kuwa katika mipango ya kuishawishi klabu ya Shakhtar Donetsk iwauzie Alex, ila uongozi wa klabu hiyo January 19 unaripotiwa kutoa taarifa za kutokuwa na mpango wa kumuuza Alex hususani katika dirisha hili dogo la usajili la mwezi January.
Staa huyo ambaye kama angejiunga Chelsea angekutana na wabrazil wenzake kama Ramires na Oscer, anatajwa kuivutia Chelsea hususani kwa wastani wake wa sasa kucheza mechi 15 akiwa na klabu ya Shakhtar Donetsk na kufunga magoli 22
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.