Mwaka 2015 Yasutaro Koide aliingia kwenye kitabu cha kumbukumbu kubwa za duniani cha Guinness World Records baada ya kuwa mwanaume mwenye umri mkubwa zaidi duniani.
Mzee huyo alizaliwa March 13, 1903 katika jiji la Nagoya, Japan na amefariki leo akiwa na umri wa miaka 112 kutokana na maradhi ya moyo na nimonia.
Mzee huyo alivalishwa rekodi hiyo mwaka 2015 baada ya kifo cha bibi Misao Okawa kutoka Japan aliyefariki akiwa na umri wa miaka 117.
Marehemu Yasutaro aliwahi kuulizwa kuhusu siri ya maisha marefu wakati akiwa hai, alisema watu waache kufanya kazi ngumu na pia waishi kwa furaha.
Mpaka sasa bado haijafahamika nani atamrithi kama mwanaume mzee zaidi baada ya yeye kufariki huku rekodi ya mtu mkongwe zaidi duniani ikishikiliwa na mwanamke Susannah Mushatt raia wa Marekani ambaye ana umri wa miaka 116.
Video yenye stori yake hii hapa pia… #RIP
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.