Ligi Kuu soka Tanzania bara iliendelea kwa michezo mitano kupigwa katika viwanja tofauti, kwa upande wa Dar Es Salaam klabu ya JKT Ruvu ilikuwa mwenyeji wa Simba katika mchezo wa 15 wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2015/2016. Simba ilikuwa mgeni huku huu ukiwa mchezo wao wa pili kucheza bila kuwa na kocha wao mkuu.
Huu ulikuwa mchezo unaozikutanisha timu iliyopo nafasi ya 11 na timu iliyopo nafasi ya nafasi ya tatu, Simba ilikuwa inahitaji point tatu ili iweze kujiweka katika nafasi nzuri ya kushindana na Yanga waliokuwa wanaongoza Ligi kwa point 36 na Azam FC wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na point 36 sema wamezidiana magoli.
Simba walikutana na JKT Ruvu ambao walionesha dalili ya kutaka kupata matokeo licha ya kuwa wapo nafasi ya 11, hadi kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliokuwa imefanikiwa kuona nyavu za mwenzake, kipindi cha pili Simba walifanya mabadiliko na kumuingiza Hassan Kessy kuchukua nafasi ya Peter Mwalyanza, mabadiliko ambayo yalionekana kuwa na faida.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu January 20
- Ndanda FC 4 – 1 Mbeya City
- Tanzania Prisons 2 – 1 Coastal Union
- Stand United 2 – 1 Toto Africans
- Mgambo JKT 1 – 2 Azam FC
Simba walifanikiwa kupata goli la kwanza kupitia kwa Hamis Kiiza dakika ya 51, baada ya kutumia vyema nafasi ya mkwaju wa penati aliyofanyiwa madhambi Danny Lyanga. Wakati JKT wanatafakari namna ya kupata goli la kusawazisha, dakika ya 61 Danny Lyanga akapachika goli la pili na kuufanya mchezo umalizike kwa Simba kuibuka na ushindi wa goli 2-0.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.