Baada ya watani zao wa jadi Simba January 20 kushuka dimbani kuvaana na JKT Ruvu katika mchezo wa 15 wa Ligi Kuu soka Tanzania bara na kuibuka na ushindi wa goli 2-0. Alhamisi ya January 21 ilikuwa ni zamu ya wapinzani wao wa jadi klabu ya Dar Es Salaam Young Africans kuivaa Maji Maji FC Wanalizombe.
Yanga wakiwa ndio wenyeji wa mchezo huo uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, waliikaribisha Maji Maji FC inayofundishwa na kocha wao mpya Kally Ongara katika jiji la Dar kwa kipigo cha goli 5-0, nidhamu ya mchezo Maji Maji waliionesha kipindi cha kwanza licha ya kuwa Thabani Kamusoko alifanikiwa kuwafunga goli dakika ya 4.
Kipindi cha pili Yanga walionekana kurudi na mbinu mbadala kwani walifanikiwa kupachika mabao mengine manne, Donald Ngoma ndio alikuwa mchezaji wa kwanza wa Yanga kwa kipindi cha pili kuziona nyavu za Maji Maji FC dakika ya 47, kabla ya Amissi Tambwe hajapachika magoli yake matatu dakika ya 58, 72 na 84 na kuufanya mchezo umalizike kwa goli 5-0. Kwa matokeo hayo Yanga bado wanaendelea kuwa juu ya Azam FC wakiwa na point 39 sawa na Azam FC ila wamewazidi magoli.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu January 21
- Mwadui FC 2 – 1 Kagera Sugar
- African Sports 0 – 0 Mtibwa Sugar
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.