Mtu wangu wa nguvu mzunguuko wa kwanza wa Ligi Kuu soka Tanzania bara umemalizika, lakini haina maana kwamba weekend hii hakuna burudani ya soka, kuna michezo kadhaa ya Kombe la FA kwa Tanzania, Ligi Kuu Uingereza na Hispania. Hii ndio ratiba ya michezo yenyewe mtu wangu.
Kesho Jumamosi ya January 23 michezo mitatu itachezwa, mjini Morogoro Burkinfaso FC watawakaribisha Simba SC katika uwanja wa Jamhuri mjini humo, Pamba FC watawakaribisha Toto Africans uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, huku Ndanda FC wakicheza dhidi ya Mshikamno FC katika uwanja wa Nagwanda Sijaona Mtwara.
Jumapili ya January 24 michuano hiyo itaendelea kwa michezo mitatu, jijini Dar es salaam Young Africans watawakaribisha Friends Rangers uwanja wa Taifa, Njombe Mji watakuwa wenyeji wa Tanzania Prisons uwanja wa Amani Njombe, huku Stand United wakicheza dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Hii ni ratiba ya Ligi Kuu Uingereza weekend hii
Jumamosi ya January 23 kwa saa za Afrika Mashariki
- Norwich Vs Liverpool Saa 15:45
- Crystal Palace Vs Tottenham Saa 18:00
- Leicester Vs Stoke Saa 18:00
- Man Utd Vs Southampton Saa 18:00
- Sunderland Vs Bournemouth Saa 18:00
- Watford Vs Newcastle Saa 18:00
- West Brom Vs Aston Villa Saa 18:00
- West Ham Vs Man City Saa 20:30
Jumapili ya January 24 ratiba kwa saa za Afrika Mashariki
- Everton Vs Swansea Saa 16:30
- Arsenal Vs Chelsea Saa 19:00
Ratiba ya Ligi Kuu Hispania
Ratiba ya Ligi Kuu Hispania kwa saa za Afrika Mashariki Jumamosi ya January 23
- Málaga Vs Barcelona Saa 18:00
- Espanyol Vs Villarrea Saa 20:15
- Granada CF Vs Getafe Saa 22:30
- Rayo Vallecano Vs Celta de Vigo Saa 00:05
Jumapili ya January 24
- Ath Bilbao Vs Eibar Saa 14:00
- Atl Madrid Vs Sevilla Saa 18:00
- Deportivo de La Coruña Vs Valencia Saa 20:15
- Real Betis Vs Real Madrid Saa 22:30
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.