Michuano ya Kombe la FA limeendelea tena leo January 24, baada ya jana kushuhudia michezo kadhaa ikichezwa ikiwemo mchezo wa Simba dhidi ya Burkinafaso katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro. January 24 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam Yanga walishuka dimbani kumenyana na Friends Rangers.
Mchezo ulianza kwa Yanga kupumzisha baadhi ya nyota wake wa kikosi cha kwanza akiwemo Amissi Tambwe, lakini ulikuwa ni mchezo wa kwanza wa kiungo wa kimataifa wa Rwanda aliyekuwa kafungiwa na Yanga Haruna Niyonzima, Yanga walianza kwa kucheza soka safi na kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa, kwani hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Yanga walikuwa mbele kwa goli 2-0.
Kipindi cha pili Yanga walirejea wakiwa na kasi na kuendelea kumiliki mpira na dakika ya 50 tulishuhudia Matheo Anthony akipachika goli lake la kwanza la mashindano toka amejiunga na Yanga, hilo lilikuwa ni goli la tatu kwa Yanga, baada ya Simon Msuva kufunga magoli mawili ya awali dakika ya 5 na 23 kipindi cha kwanza. Hadi dakika 90 zinamalizika waliibuka na ushindi wa goli 3-0.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.