Najua kuna watu huenda wako njiani au wana mipango ya kusafiri kwenye mji ambao una headlines za vikao vya Bunge kwa sasa, Dodoma town.. au wengine wana safari kwenda mikoa mingine kupitia mkoa huo.
Naomba nikufahamishe kwamba kuna sababu za kuwa na umakini wa ziada unapokuwa barabarani, kama unatumia barabara ya Morogoro-Dodoma eneo la Kibaigwa kuna uharibifu umetokea na kama mvua ikiendelea kupiga kabla ukarabati haujafanyika basi hali huenda ikawa mbaya zaidi.
Mvua imenyesha na kumetokea uharibifu wa baadhi ya sehemu, pengine inapita gari moja tu yani haziwezi kupishana mbili kwa wakati mmoja.
Picha zote nimezitoa >>> Michuzi Blog
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE