Mkali wa Bongo Fleva anayemiliki headlines na Air Time kwa hit single yake ya ‘Mama Kijacho’ Khalid Ramadhani maarufu kama Tunda Man amerudi kwenye headlines February 6 baada ya kuanza rasmi utekelezaji wa majukumu yake ya ubalozi wa kampeni ya Amsha Mama.
Tunda Man ameanza shughuli zake za kibalozi kwa kuwatembelea wakinamama wafanyabiashara wadogo wadogo wa Tandale Dar Es Salaam, Tunda Man alifanya ziara hiyo ya kushitukiza akiwa na boss wa label ya Candy and Candy Records na waandaaji wa tamasha la AFWAB AMSHA MAMA AFRIKA Joe Kariuki.
Tamasha la AFWAB AMSHA MAMA linatarajiwa kufanyika March 25-27 Naivasha Kenya, Tunda Man na Kairuki wote kwa pamoja waliwapa wakinamama hao laki moja moja kila mmoja, ikiwa ni sehemu ya lengo lao la kuinua wakinamama, Tunda Man amepewa ubalozi waandaaji wa tamasha la AFWAB AMSHA MAMA .
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwapia ungana na MillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.