Uganda ilikua kwenye uchaguzi mkuu wa kumchagua Rais na Wabunge juzi ambapo matokeo ya awali yalianza kutolewa kuanzia jana lakini leo matokeo kamili yametolewa na Yoweri Museveni ambaye amekuwepo kwenye kiti cha Urais toka mwaka 1986 ametangazwa mshindi huku mpinzani wake mkuu ambaye ni Kizza Besigye akikataa matokeo hayo aliyoyaita ya wizi wa kura.
VIDEO: Electoral Commission declares Yoweri Kaguta Museveni as president elect in the 2016 elections. #UgandaDecides pic.twitter.com/ufzC4lqGkG
— NBS Television (@nbstv) February 20, 2016
Kituo cha TV cha NBS kimeripoti kwamba huduma za Taxi mitaani, mitandao ya kijamii na huduma za benki za simu za mkononi zimerejea baada ya serikali kuamuru juzi kila kitu kizimwe kuanzia Facebook, Twitter, Whatsapp.
Rais Museveni baadae alihojiwa na kusema mitandao ya kijamii ilizimwa kwa muda mfupi tu na watu hawakutakiwa kuwa na hofu sababu ilifanywa ili kuzuia upotoshaji wa taarifa tu ambao umekua ukifanywa mara kwa mara.
Museveni: Blocking of social media sites and MM services done in the interest of national security #UgandaDecides pic.twitter.com/2NEA4N4Xvh
— NBS Television (@nbstv) February 18, 2016
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE