Jeshi la Polisi Dar es salaam linawahoji baadhi ya wanasiasa kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), pia yupo Mbunge wa Kawe Halima Mdee kwa tuhuma za kuhusika na vurugu zilizotokea siku iliyohairishwa kufanyika kwa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar.
Nje ya jengo la Polisi Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Prof Abdallah Safari amezungumza na AYO TV na kusema>>>‘Halima ameshitakiwa kwa kosa la shambulizi la mwili ambalo kisheria ni kosa dogo, wanasema alimshambulia RAS wakati wa uchaguzi ulipoahirishwa pale karimjee hall juzi’
‘kwa hiyo nimekuja kushuhudia maelezo yake akiandika kwa maoni yangu halima hakuhusika kabisa na hicho kitu lakini kama kawaida ya polisi wamemkatalia dhamana kwa hiyo halima atalala rumande leo’
Unaweza kuitazama hii Video siku vurugu hizo zilivyotokea….
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE