Hii ni dunia ambayo kila siku kuna watu wanafanya utafiti wa vitu duniani… sasa leo March 4 2016 nakuletea matokeo ya utafiti uliofanywa kwenye bara la Afrika na kuonyesha kwamba ifuatayo ndio miji kumi ya nchi za Afrika ambako Matajiri wengi wanapatikana.
Kila tajiri aliejumuishwa kwenye hii list ni yule aliye na utajiri unaozidi dola za kimarekani milioni 30 ambazo kwa Tanzania ni zaidi ya BILIONI 65 ambapo moja ya miji hiyo 10 Dar es salaam ipo pia ikiwa nafasi ya sita ikiwa na matajiri 36 wenye utajiri huo.
List kamili kwenye nafasi ya kumi ni mji wa 10. Kano Nigeria, 9– Marrakesh Morocco 8– Addid Ababa Ethiopia 7– Abuja Nigeria 6– Dar es salaam Tanzania 5– Nairobi Kenya ambako kuna matajiri wa aina hiyo wapatao 69. Namba 4 ni Capetown South Africa yenye matajiri 115 wa aina hiyo. 3- Lagos Nigeria yenye 131 2- Cairo Egypt 1. Johannesburg South Africa yenye matajiri wa aina hiyo 238.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE