Uchaguzi wa Meya Dar es salaam unazidi kuchukua headline kila siku. Ikiwa ni siku moja tangu kuachiliwa kwa dhamana baadhi ya Wabunge na Madiwani wa Chadema kwa kosa la kumjeruhi Katibu tawala Mkoa wakati wa uchaguzi wa Meya wa jiji la Dar es salaam ulipoahirishwa February 27 2016.
Leo March 4 2016 baadhi ya Wabunge na Madiwani wa Ukawa Dar es salaam wamefika ofisi ya Halmashauri ya Jiji, ili kutaka kujua tarehe na siku ipi uchaguzi wa Meya utafanyika. Mwenyekiti wa Mkoa Dar es Salaam ‘Chadema‘ na mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Mwikabe Waitara ameeleza kuwa muda wa kisheria kumpata Meya wa jiji ulishaisha, kwani ilitakiwa siku 90 baada ya uchaguzi wa madiwani kufanyika, Meya awe amekwishapatikana na hata siku 30 zilizoongezwa zimeisha pia.
>>> ‘tumekuja hapa kwa amani sana na mkurugenzi atupe majibu leo na wasipotoa wiki ijayo kwa wakati fulani, siku fulani na kwa masaa fulani tutakuja hapa kwa utaratibu mwingine, hiyo tarehe kama tunafanya uchaguzi hapa tufanye ili Tanzania na dunia ijue kinachofanyika hapa ni uonevu’;- Mwita Mwikabe Waitara
Licha ya juhudi hizo za Baadhi ya Wabunge na Madiwani wa Ukawa kufika katika ofisi hizo hawakupata nafasi ya kuonana na Mkurugenzi ili kupata majibu ya Tarehe ya uchaguzi wa Meya.
Hii ndio full Video ya tukio lenyewe….
Unaweza kuitazama full video siku ya uchaguzi ulipoahirishwa….
Nini maoni yako kuhusu maamuzi haya ya UKAWA?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE