March 20 2016 ni siku ambayo Uchaguzi wa marudio Zanzibar utafanyika, zikiwa zimebaki siku chache kufanywa kwa uchaguzi huo, matukio mbalimbali yamekuwa yakichukua vichwa vya habari ikiwamo nyumba ya Kamshina wa polisi kulipuliwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu.
Leo March 17 2016 Chama cha Wananchi CUF wamejitokeza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam kupitia Naibu katibu Mkuu Magdalena Sakaya kuitaka Serikali iingilie kati vitendo vinavyofanywa na watu wanaojiita ‘mazombi’ kwa kuwapiga wananchi na wafuasi wa chama hicho, aidha wamewashutumu polisi kwa kuwashikilia viongozi wa chama hicho bila sababu…
>>>’Kumekuwa na vikundi viovu vikiwavamia wafuasi wa CUF na kuwapiga pamoja na kuwajeruhi, maarufu kwa jina la mazombi jeshi la polisi mpaka leo hii hawajakamata Zombi hata mmoja na wanasema kwamba hao mazombi hawawajui na hawapo, lakini cha kushangaza kila tukio baya likitokea Zanzibar wanasingiziwa wafuasi wa CUF‘:-Magdalena Sakaya
>>>’kila siku viongozi wa CUF wanakamatwa na mpaka hivi sasa wafuasi wa CUF zaidi ya 60 wamekamatwa wakisingiziwa kuhusika na uvunjifu wa amani‘:-Magdalena Sakaya
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
Ilikupita hii Video ya Kilichomchekesha Rais Magufuli japokuwa alikua kavaa sura ya kazi IKULU