Ni March 20, 2016 ambapo chama cha mapinduzi kilifanya mkutano na waandishi wa habari na kumtangaza msemaji mpya wa chama cha mapindizi baada ya waziri Nape kuteuliwa kufanya kazi za uwaziri kulitumikia taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari katibu mkuu wa chama hicho, ndugu Abdulrahman Kinana alisema…‘Bw.Christopher Sendeka yeye sasa ndio atakuwa msemaji wa chama cha mapinduzi kwasababu gani, kwasababu katibu mwenezi wa chama chetu ndugu Nape aliteuliwa kuwa waziri wa Serikali na Waziri wa habari utaratibu wa chama chetu nafikiri ni busara mtendaji wa chama anapoteuliwa kuwa waziri basi atajishughulisha na kazi yake ya uwaziri lakini kwasababu katibu mwenezi ameteuliwa na halmashauri kuu ya taifa, uteuzi wake unateguliwa tu na halmashauri kuu kama alivyoteuliwa na halmashauri ya kitaifa’ – Kinana
‘Kwahiyo hakuna mwenye mamlaka wa kutengua uteuzi wake isipokuwa halmashauri ya kitaifa kwahiyo atabaki kwa jina kuwa mwenezi wa chama chetu mpaka hapo halmashauri kuu itakapokaa kutengua nafasi hiyo aliyonayo ya mwenezi, lakini tungependa kazi ya kuisemea chama cha mapinduzi kiendelee kwahiyo tumemteua bwana Christopher Ole Sendeka kuwa msemaji wa chama chetu’ – Kinana
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, InstagramnaYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE