Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI, George Simbachawene ametangaza leo March 21, 2016 kuwashughulikia wale wote wanaofanya hujuma katika sekta ya elimu nchini, wakiwemo Walimu wanaokimbia sehemu zao za kazi hususani vijijini na kukimbilia mijini.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo March 21, 2016 alisema…‘Katika eneo la upangaji wa Walimu ni tatizo kubwa na nadiliki kusema hadharani kwamba upangaji wa walimu kwenye shule zetu ni wa ovyo leo hii tunaupungufu wa ualimu kwenye vijiji kwa asilimia zaidi ya 40% na ongezeko la walimu mijini ni kama asilimia 50% kwa maana ya kwamba walimu wengi wapo Dar es Salaam, walimu wengi wapo kwenye miji mikubwa makao makuu ya mikoa na makao makuu ya wilaya’ – George Simbachawene
‘Hata wanawake wanasema wanafuata wanaume zao huko ni kukosa uzalendo kama ulikubali kuajiliwa lazima ukubali kufanya kazi mahala popote pale na watanzania ni wote mpaka waliopo kule vijijini haiwezekani kukubali kazi mjini na kukataa kijijini’ – George Simbachawene
itazame hii hapa video fupi
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE