Klabu ya soka ya Simba March 23 kupitia kwa mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu yao Haji Manara wamethibitisha kukabidhi barua yao ya malalamiko kwa shirikisho la soka Tanzania TFF, inayowatuhumu TFF kuwapendelea Yanga na Azam FC katika ratiba ya Ligi.
Manara ameweka wazi barua hiyo na kueleza kuwa baada ya hapo anaipeleka nakala kwa waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye ili kuvisukuma vyombo husika kutenda haki, kwani Yanga imekuwa ikipendelewa kwa mambo mengi.
Hata hivyo Manara amethibitisha kuwa Simba imempa barua inayomtaka Abdi Banda ajieleze, kwani asipewe adhabu na klabu kutokana na kuonesha utovu wa nidhamu kwa kocha Jackson Mayanja na kugoma kuvaa jezi zenye nembo ya mdhamini.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE